101

1 Inayo gonga!
2 Nini Inayo gonga?
3 Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
4 Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
5 Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
6 Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
7 Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
8 Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
9 Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
10 Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
11 Ni Moto mkali!