102

1 Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
2 Mpaka mje makaburini!
3 Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
4 Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
5 Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
6 Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
7 Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
8 Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.