104

1 Ole wake kila safihi, msengenyaji!
2 Aliye kusanya mali na kuyahisabu.
3 Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!
4 Hasha! Atavurumishwa katika H´ut´ama.
5 Na nani atakujuvya ni nini H´ut´ama?
6 Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.
7 Ambao unapanda nyoyoni.
8 Hakika huo utafungiwa nao
9 Kwenye nguzo zilio nyooshwa.