114

1 Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu,
2 Mfalme wa wanaadamu,
3 Mungu wa wanaadamu,
4 Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,
5 Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,
6 Kutokana na majini na wanaadamu.