93

1 Naapa kwa mchana!
2 Na kwa usiku unapo tanda!
3 Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
4 Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
5 Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
6 Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
7 Na akakukuta umepotea akakuongoa?
8 Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
9 Basi yatima usimwonee!
10 Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
11 Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.