94

1 Hatukukunjulia kifua chako?
2 Na tukakuondolea mzigo wako,
3 Ulio vunja mgongo wako?
4 Na tukakunyanyulia utajo wako?
5 Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
6 Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
7 Na ukipata faragha, fanya juhudi.
8 Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.