95

1 Naapa kwa tini na zaituni!
2 Na kwa Mlima wa Sinai!
3 Na kwa mji huu wenye amani!
4 Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
5 Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
6 Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
7 Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
8 Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?