97

1 Hakika Sisi tumeiteremsha Qur´ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.
2 Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
3 Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
4 Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
5 Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.