109

1 Sema: Enyi makafiri!
2 Siabudu mnacho kiabudu;
3 Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
4 Wala sitaabudu mnacho abudu.
5 Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
6 Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.