99

1 Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
2 Na itakapo toa ardhi mizigo yake!
3 Na mtu akasema: Ina nini?
4 Siku hiyo itahadithia khabari zake.
5 Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
6 Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
7 Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
8 Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!