100

1 Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
2 Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
3 Wakishambulia wakati wa asubuhi,
4 Huku wakitimua vumbi,
5 Na wakijitoma kati ya kundi,
6 Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
7 Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
8 Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
9 Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
10 Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
11 Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!