110

1 Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,
2 Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,
3 Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.